domingo, 5 de febrero de 2012

Dyslexia ni nini hasa?

Dyslexia ni tofauti tatizo ambalo linaweza kuleta shida katika...

• Kusoma, tahajia na kuandika.
• Ujuzi wa numerali, kama vile kufanya hesabu, hisabati za akilini, chati za hesabu.
• Kuweza kuwa makini, kuweza kuyafikia makataa na mpangilio wa kibinafsi wa mambo.
• Kumbukumbu.
• Kupanga vitu, kama vile kuweka tarehe na nambari katika mpangilio ulio sahihi.
• Kumakinikia jambo.

Mtu mmoja kati ya watu 10 miongoni mwetu hukumbwa na aina fulani ya dyslexia.
Watu wengi mashuhuri na waliofanikiwa huishi na tatizo hili la dyslexia. Watu wanaokumbwa na tatizo la dyslexia wanaweza kuwa…

• Wabunifu na wenye uwezo wa kifikiri.
• Wanaweza kusuluhisha matatizo.
• Wavumbuzi.
• Wanaweza kuwasiliana vizuri.

Ikiwa una wasi wasi wewe mwenyewe au juu ya mwanao kwamba huenda wewe au yeye amekumbwa na tatizo hili, mnaweza kupata usaidizi na habari za kina kutoka …



Fuente: British Dyslexia Association

Porque la dislexia también habla en swahili.